Storm FM
Storm FM
13 April 2025, 1:56 pm

Ubovu wa barabara ya kwenda katika hospitali ya Katoro wawaibua wananchi wa kata za Katoro na Ludete wawaibua wananchi
Na Mrisho Sadick:
Wakazi wa Kata ya Ludete mamlaka ya mji mdogo wa Katoro wilayani Geita wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kutengeneza barabara inayoelekea kwenye Hospitali ya Katoro kutokana na barabara hiyo kuharibika vibaya.

Wananchi hao wametoa kilio hicho wakati wakizungumza na Channel Ten ambapo wamesema wanapata changamoto kuwafikisha wagonjwa kwenye hospitali hiyo kutokana na barabara zote zinazoingia eneo hilo kuharibiwa vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Nicholous Kasendamila amefika katika Hospitali hiyo kuangazia changamoto hiyo nakumuagiza Meneja wa TARURA wilaya ya Geita Mhandisi Bahati Subeya kwa njia ya simu kuhakikisha anatatua changamoto hiyo haraka.