Storm FM
Storm FM
4 April 2025, 2:39 pm

Serikali inatakiwa kuweka mkazo kwenye utatuzi wa changamoto ya matibabu bila malipo kwa wazee kwani wengi wao wamekuwa wakikosa fursa hiyo.
Na Mrisho Sadick:
Mzee Ernest Gabriel Mkazi wa Kijiji cha Kasota Kata ya Bugulula wilayani Geita anaesumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu amedai kufukuzwa nakunyimwa huduma kwenye Kituo cha Afya Kasota kwa madai kuwa hana barua Kutoka Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji hicho.
Mzee Gabriel anaeishi katika mazingira magumu ametoa malalamiko hayo April 04,2025 kwenye Mkutano wa hadhara wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita aliyefika kwenye Kijiji hicho kusikiliza nakutatua kero za wananchi huku akihoji Kwanini hapewi huduma bure licha ya serikali kusisitiza wazee kutibiwa bila malipo.

Mganga mfawidhi wa Kituo Cha Afya Kasota Dkt Enos Jumanne amekiri kumtambua Mzee huyo nakwamba hakuwapatiwa huduma kwenye Kituo hicho kwakuwa hana barua Kutoka Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Nicholaus Kasendamila akamtaka Mtendaji wa Kijiji hicho kumpatia barua Mzee huyo kwenye Mkutano huo Ili awe kwenye Mpango wa wazee wanaopatiwa huduma bila malipo huku akimuagiza Mkuu wa wilaya ya Geita kusimamia suala hilo.