Storm FM

Rais Samia atoa zawadi kwa watoto yatima Geita

31 March 2025, 3:48 pm

Mkuu wa nko wa Geita akifurahi na watoto yatima. Picha na Mkuu wa mkoa wa Geita. Picha Mrisho Sadick

Katika sikukuu hii ya Eid na Pasaka Rais Dkt Samia ameebdelea kuwakumbuka watoto wenye uhitaji ikiwemo yatima.

Na Mrisho Sadick:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi zenye thamani ya zaidi ya milioni 13 kwa ajili ya sikukuu ya Eid na Pasaka kwenye vituo vitatu vya kulelea watoto yatima katika manispaa ya Geita Mkoani Geita.

Katika baridi ya upweke na majonzi ya kukosa malezi ya wazazi watoto hawa wameonesha nyuso zenye nuru baada ya Rais Dkt Samia kuwakumbuka.

Mkuu wa mkoa wa Geita aliyevaa suti akikabidhi zawadi ya chakula kwa watoto yatima. Picha na Mrisho Sadick

Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amekabidhi zawadi hizo kwaniaba ya Rais kwa vituo vitatu Neema House , Neema Liwali na Moyo wa Huruma lilipofanyika zoezi hilo la kugawa zawadi hizo.

Taarifa zaidi na Mrisho Sadick:

Sauti ya stori nzima