

31 March 2025, 3:34 pm
Waumini wa dini ya Kiislamu Nchini leo Jumatatu wanasherekea sikukuu ya Eid Al Fitr huku siku hii ikiwa imetaliwa na ujumbe tofautitofauti.
Na Mrisho Sadick:
Waumini wa dini ya kiislamu Mkoani Geita wametumia swala ya Eid Al Fitr kuwaombe watu waliotangulia mbele za haki kwakuwa walifanya kazi kubwa katika jamii ikiwemo ya kueneza dini hiyo.
Ibaada hiyo imefanyika katika msikiti Mkuu wa Ijumaa Manispaa ya Geita Mkoani Geita huku Katibu wa Baraza la mashekhe wa Mkoa wa Geita Bashiru Haruna amesema miongoni mwa walioguswa na Dua hiyo ni wazazi , wazee , viongozi wa dini na watu wengine wa dini hiyo waliotangulia mbele za haki.
Kwa upande wake Shekhe wa Mkoa wa Geita Al Haji Yusuph Kabaju amewataka waislamu Mkoani Geita kusherekea sikukuu hiyo kwa utulivu.