

26 March 2025, 5:38 pm
Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuhusu usafirishaji wa dhahabu kwa njia ya magendo wilayani Bukombe Mkoani Geita.
Na Mrisho Sadick:
Watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Geita Kwa tuhuma za kusafirisha dhahabu yenye thamani ya zaidi ya milioni 749 kwa njia za magendo Wilayani Bukombe.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Adam Maro ametoa taarifa hiyo wakati akizungumza na waandishi wa Habari nakwamba watu hao walikamatwa Machi 24, 2025 majira ya saa 5 usiku katika mtaa wa Kapera wilayani Bukombe na niwakazi wa mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Simiyu wakiwa na gramu 3,263 za dhahabu yenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 749.
Kamanda maro amewataja Watu hao kuwa ni Yohana Idama (34), mkazi ya Mwanza, Moshi Manzili (26) mkazi wa Simiyu, na Hamidu Salum (25) mkazi wa Shinyanga walikamatwa wakiwa na dhahabu hiyo kwenye gari aina ya Toyota Premio yenye namba za usajili T.739 EEH.
Katika tukio lingine Kamanda Maro amesema mtoto mwenye umria wa miaka 9 Ibrahim Masumbuko mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kakoyoyo Wilayani Bukombe amefariki dunia baada ya kupigwa na radi.