Storm FM

Sakata la dabi ya Kariakoo latua Geita

24 March 2025, 12:55 pm

Rajabu Mohamed (kati) mratibu wa matawi ya klabu ya Yanga mkoani Geita. Picha na Edga Rwenduru

“Wanachama na mashabiki wa Yanga ndani ya mkoa wa Geita, tunaungana na viongozi wetu wa makao makuu, hatuhitaji busara kutatua mgogoro huu unaoendelea” – Rajabu Mohamed

Na: Edga Rwenduru – Geita

Uongozi wa matawi ya wanachama wa klabu ya soka ya Yanga SC mkoa wa Geita Machi 22, 2025 umetoa msimamo wao juu ya taarifa ya bodi ya ligi waliyoitoa Machi 08, 2025 kuusu kuhairisha mechi ya Derby ya Kariakoo kati ya Yanga dhidi ya Simba SC.

Wanachama na mashabiki hao wa Yanga wakizungumza na waandishi wa habari wamesema walipata hasara kubwa kutokana na kuhairishwa kwa mechi hiyo huku wakiitaka bodi ya ligi ijiuzulu kutokana na kushindwa kusimamia na kutafsiri kanuni zinazosimamia ligi kuu.

Sauti ya mratibu wa matawi ya Yanga SC Rajabu Mohamed

Nao baadhi ya viongozi wa matawi ya Yanga mkoani Geita wamesema wanaunga mkono taarifa iliyotolewa na klabu yao kutoka makao makuu jijini Dar es salaam.

Sauti ya viongozi wa matawi ya Yanga SC Geita