

21 March 2025, 10:45 am
Mwanaume mmoja mkazi wa kata ya Kasamwa katika halmashauri ya manispaa ya Geita amenusurika kifo baada ya kufanya jaribio la kujiua kwa kunywa sumu.
Na: Kale Chongela – Geita
Gerevas Deus anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 28 mkazi wa kijiji cha Mbugani kata ya Kasamwa, halmashauri ya manispaa ya Geita amenusurika kifo baada ya kufanya jaribio la kunywa sumu baada ya mke wake kutoweka nyumbani waliopokuwa wanaishi.
Baadhi ya ndugu wa mke wake wakiwa katika ofisi ya serikali ya mtaa wamesema kijana huyo alikwenda nyumbani kwao na mke wake waishio mtaa wa Mpomvu ili kuulizia kama amekwenda huko.
Baada ya kugundua kuwa mkewe hajafika nyumbani kwao ndipo akaamua kuchukua uamuzi wa kunywa sumu akiwa katika mtaa huo kama anavyoeleza mama mzazi wa mke wake.
Balozi wa shina 3 katika mtaa wa Mpomvu Bw. Andrea Machibula ameeleza namna alivyopata taarifa juu ya tukio hilo.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mpomvu Bw. Charles Manyanga amethibitidha kutokea tukio hilo na kwamba baada ya kijana huyo kuhojiwa amekiri kuwa alikunywa sumu mara baada ya kugundua kuwa mke wake wakati anaondoka alichukua kiasi cha fedha za kitanzania shilingi Laki mbili jambo ambalo kwake lilimpa wakati mgumu.