

21 March 2025, 9:55 am
Wakazi wa mtaa wa Mpomvu kata ya Mtakuja, halmashauri ya manispaa ya Geita wameshtushwa na hali ya mti uliopo katika kanisa la GGC uliokuwa umekatwa kukutwa umesimama.
Na: Kale Chongela – Geita
Wakizungumza na Storm FM Marchi 20, 2025 baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema Marchi 19, 2025 majira ya jioni mti huo ulikuwa upo chini baada ya kuwa umekatwa na hivyo wameshangaa kuona ukiwa umesimama tena.
Mchungaji wa kanisa lililopo karibu na mti huo Bw. Jefta Lameck amesema mti huo ulidodoshwa na upepo ulioambatana na mvua na ndipo akatafutwa mtu wa kuukata na baada ya kuuta usiku wa kuamkia leo wamekuta umesimama.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bw. Charles Manyanga amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kuacha Imani potofu huku Jeshi la Polisi likifika eneo hilo na kuwatawanya wananchi na kuwashi waendelea na majukumu yao.