

19 March 2025, 5:58 pm
‘Inabidi viongozi wa mtaa waweke wazi juu ya mapato ya asilimia 10 ili tuelewe inatumika katika maeneo gani’ – Mwananchi
Na: Kale Chongela – Geita
Baadhi ya wakazi wa kata ya Buhalahala katika halmashauri ya manispaa ya Geita wamewaomba viongozi wa serikali za mitaa katika maeneo yao kuwasilisha asilimia 10 ofisini zinazotokana na wananchi kutoa baada ya kuuza au kununua maeneo yao.
Hayo yamebainishwa leo Marchi 19, 2025 na baadhi ya wakazi wa mtaa wa Shilabela kata ya Buhalahala wakieleza kuwa ipo haja ya viongozi wa serikali za mitaa kuhakikisha fedha zinazopatikana katika manunuzi ya maeneo (viwanja) zinawasilishwa ofisini ili zitumike katika maendeleo ya mtaa husika hasa katika ujenzi wa ofisi.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Shilabela Bw. Fredrick Andrea Masalu Nzigula amesema suala la asilimia 10 ya malipo katika viwanja halipo kwenye utaratibu wa kwamba halina ulazimika wowote wa mwananchi kutoa pindi anaponunua eneo.