Storm FM

Wakazi wa Nyamakale wawatupia lawama viongozi wa mtaa

6 March 2025, 4:23 pm

Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa mtaa ulioitishwa na mwenyekiti. Picha na Kale Chongela

Kufuatia kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu katika mtaa wa Nyamakale uliopo kata ya Nyankumbu katika halmashauri ya manispaa ya Geita, wananchi wawatupia lawama viongozi wa mtaa.

Na: Kale Chongela – Geita

Wakazi wa mtaa wa Nyamakale, kata ya Nyankumbu halmashauri ya manispaa ya Geita wamedai kukosa imani na viongozi wa serikali ya mtaa huo kufutia kutotimiza majukumu ya wananchi ikiwemo kusimamia suala la ulinzi na usalama wa mtaa huo.

Hayo yamebainishwa leo Marchi 06, 2025 na baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara ambapo wamesema kuwa changamoto ya viongozi hao wa mtaa huo wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea hali ambayo inasababisha kushindwa kusimamia suala la ulinzi shirikishi wa mtaa na kupelekea vitendo vya uhalifu.

Sauti ya wananchi

Baadhi ya mabalozi wa eneo hilo wamesema licha ya jitihada kubwa ambazo wanazifanya hasa kwa kushirikiana na baadhi ya wananchi  zimekuwa zikigonga mwamba kutokana na viongozi wa serikali ya mtaa kutotoa ushirikiano.

Sauti ya mabalozi wa mtaa

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bw. Henry Tito Mkengela amesema changamoto kubwa iliyopo katika mtaa huo ni kutokana na ushirikiano hafifu kati yake na afisa mtendaji 

Sauti ya mwenyekiti Henry Tito

Jitihada za kumtafuta mtendaji wa mtaa huo Bi. Irene Fumbo zimefanikiwa ambapo ameeleza kuwa hayuko sawa kuzungumza kwa hivi sawa.

Muonekano wa ofisi ya serikali ya mtaa wa Nyamakale. Picha na Kale Chongela