

5 March 2025, 12:27 pm
Hadi kufikia Desemba 2022 jumla ya wakulima 6,323 na eneo la ekari 11,896 lilikuwa limetengwa kwa ajili ya kilimo cha alizeti Geita, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza uzalishaji na kujitosheleza kwa mafuta ya kula nchini.
Na: Daniel Magwina – Geita
Mamlaka ya Nafaka na Mazao mchanganyiko nchini (COPRA) imekabidhi zaidi ya tani hamsini za mbegu za alizeti mkoani Geita kwa ajili ya kugawiwa kwa wakulima mkoani Geita bure.
Ugawaji huo umefanyika Machi 04, 2025. Akizungumza mwakilishi wa Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Bi. Sezaria Makota wakati akikabidhi mbegu hizo kwa mkuu wa mkoa wa Geita amesema:
Akizungumza baada ya kupokea mbegu hizo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martin Reuben Shigela amewapongeza COPRA kwa kuleta mbegu bora kwa wakulima kwa ajili ya zao la alizeti
Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa wilaya wa mkoa wa Geita, Mkuu wa Wilaya ya Geita Hashim Komba amesema watahakikisha wakulima wanapata mbegu hizo ili ziweze kuleta tija iliyo kusudiwa.
Nao baadhi ya wakulima lutokea wilaya mbalimbali mkoani hapa wameelezea jinsi watakavo simamia mbegu hizo.