Storm FM

Adaiwa kutaka kujiua baada ya kugombana na mke wake

22 February 2025, 11:41 am

Muonekano wa genge la Miti mirefu, Msalala road. Picha na Amon Mwakalobo

Migogoro ya familia hususani baina ya mke na mue imeendelea kutajwa kuwa kikwazo cha maendeleo kutokana na mifarakano ambayo wanandoa hupitia.

Na: Amon Mwakalobo – Geita

Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Nehemia ambaye ni mkazi wa Msalala road, halmashauri ya manispaa ya Geita mkoani Geita anayefanya biashara ya kuuza kuku katika genge la Miti mirefu amenusurika kifo baada ya kudaiwa kujidunda sindano yenye sumu kwa lengo la kujiua huku chanzo kikielezwa kuwa ni mke wake kutoroka nyumbani na watoto baada ya Ugomvi wa muda mrefu katika familia yao.

Tukio hilo limetokea asubuhi ya Februari 18, 2025 ambapo kwa mujibu wa majirani mwanaume huyo alipozidiwa akaamua kujipeleka mwenyewe hospitali kwaajili ya kupata matibabu ili kunusuru roho yake.

Balozi wa shina namba tano Bi. Angelina Gervas amesimulia jinsi tukio hilo lilivotokea na hatua walizozichukua.

Sauti ya balozi Angelina Gervas

Baadhi ya majirani ambao anaishi nao wameeleza wanachofahamu juu ya tukio hilo huku wakitoa rai kwa watu kuacha tabia ya kujidhuru pindi wanapopitia changamoto.

Sauti ya majirani

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bw. Sostenes Kalist amewataka wananchi wa mtaa huo kutojichukulia sheria mkononi ikiwemo kujiua kwani hata maandiko matakatifu yanasema kujiua ni dhambi.

Sauti ya mwenyekiti Sostenes Kalist