Storm FM

Bampa la choo lapasuka na kutiririsha maji Uwanja

19 February 2025, 12:56 pm

Muonekano wa shimo la choo baada ya mvua kunyesha mtaa wa Elimu. Picha na Paul William

Inaelezwa kuwa bampa la choo cha nyumba yenye wapangaji limegongwa na gari na kupelekea kuangukia ndani ya shimo la choo.

Na: Paul William – Geita

Tukio hilo limetokea mtaa wa Elimu, kata ya Nyankumbu, halmashauri ya manispaa ya Geita ambapo February 17, 2025 mvua ilinyesha kwa baadhi ya maeneo manispaa ya Geita na kupelekea shimo la choo hicho kujaa maji na kuchangamana na maji ya mvua kisha kusambaa kwenye mtaa huku ikielezwa kuwa baada ya mvua kunyesha kuna watoto waliokuwa wakichezea maji hayo.

Wakazi wa nyumba hiyo hawakupatikana baada ya madhira hayo ambapo Storm FM imempata jirani wa nyumba hiyo ambaye anaeleza juu ya changamoto hiyo

Sauti ya Jirani Henry Chasama

Balozi wa shina namba tatu katika mtaa huo wa Elimu ameeleza hajapewa malalamiko hayo huku akieleza wakazi wa nyumba hiyo akiwemo mwenye nyumba hawajafika kwake kwaajili ya kujitambulisha

Sauti ya Balozi

Mwenyekiti wa mtaa wa Elimu Hassan Mshole amesema suala hilo halifahamu kwani halijafika ofisini kwake.

Sauti ya mwenyekiti Hassan Mshole

Hata hivyo, inaelezwa kuwa katika mtaa jirani wa Uwanja kata ya Nyankumbu, mvua hiyo ilipelekea madhara ya mti kuangukia nyumba na kuiboa ambapo hakuna madhara ya kibinadamu yaliyojitokeza isipokuwa uharibifu wa miundombinu.

Muonekano wa nyumba ikiwa imeangukiwa na mti baada ya mvua kunyesha. Picha na Paul William