

10 February 2025, 11:53 am
Vitendo vya wizi wa mifugo aina ya ng’ombe vinaendelea kuchukua sura mpya mkoani Geita ambapo matukio hayo yameendelea kujitokeza hali inayochochea hasira za wananchi.
Na: Amon Mwakalobo – Geita
Mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 45 ameuawa na wananchi wenye hasira kali katika kitongoji cha Kasenyi, kata ya Nyakamwaga, kijiji cha Iponyamakalai wilayani na mkoani Geita baada ya kukutwa akiwa na nyama ndani ya mifuko akisadikiwa kushirikiana na baadhi ya watu kuchinja ng’ombe wanaodaiwa kuibwa kutoka kwenye kaya ya mmoja wa wananchi katika kijiji hicho.
Tukio hilo limetokea alfajiri ya kuamkia februari 08, 2025 ambapo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kitongoji hicho amesema alipigiwa simu na wananchi kumueleza juu ya tukio hilo, huku akitupa lawama kwa watu wanaofanya vitendo vya wizi.
Sikudhani Shija ni mke katika familia iliyoibiwa mifugo yao ambapo anaeleza namna alivyofahamu juu ya tukio hilo.
Jirani wa familia iliyoibiwa Mariam Bugalama ameeleza namna alivyosikitishwa na tukio hilo akieleza kuwa matukio hayo yamekuwa ya kujirudia kila siku katika eneo hilo.
Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo Banza Luchapa ameeleza namna alivyoshuhudia juu ya tukio hilo ambapo anaeleza ilikuwa majira ya saa tisa usiku.
Storm FM tunaendelea na jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi mkoa wa Geita kufahamu mikakati ya Jeshi la polisi katika kukabiliana na vitendo vya wizi mkoani Geita.