

4 February 2025, 12:32 pm
Februari 03, 2025 imehitimishwa wiki ya sheria nchini ambapo sambamba na hilo pia msaada wa kisheria wa Mama Samia Legal Aid umekamilika katika mkoa wa Geita.
Na: Kale Chongela – Geita
Migogoro ya ndoa katika kijiji cha kaseme, halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale, mkoani Geita imetajwa kuwa chanzo cha kudidimiza uchumi wa familia pindi inapojitokeza.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wanawake wa kijiji hicho katika mkuatano wa hadhara katika hitimisho la kampeni ya msaada wa kisheria wa mama samia ambapo wameeleza chanzo kikubwa ni wanaume kuzaa nje ya ndoa hali ambayo inaondoa maelewano katika familia
Baadhi ya wanaume wameeleza kuwa migogoro ya familia inachochewa na vitu vingi ikiwemo mfumo dume pamoja na vikundi mbalimbali ambavyo hurubuni baadhi ya wanawake na kupelekea mabadiliko yao kitabia.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kaseme Bw. Michael Kashindye amekiri uwepo kwa migogoro ya kifamilia katika kijiji chake akieleza kuwa elimu iliyotolewa uitasaidia kuweza kuepusha migogoro hiyo.
Kwa upande wake wakili msomi kutoka timu ya wataalamu wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Bw Yessey Lubunda amesema matatizo mengi katika Jamii huanzia katika ngazi ya familia na hivyo kupitia kampeni hiyo itakuwa chachu ya kleta mabadiliko