Storm FM

Manispaa ya Geita yapitisha bajeti ya Bilioni 68.3

30 January 2025, 4:03 pm

Madiwani wakiwa katika kikao cha kupitisha rasimu ya bajeti ya 2025/26. Picha na Ester Mabula

Baraza la madiwani la halmashauri ya manispaa ya Geita leo Januari 30, 2025 limejadili na kupitisha rasimu ya makadirio bajeti kwa mwaka 2025/2026 kiasi cha shilingi bilioni 68,393,812,906.00.

Na: Ester Mabula – Geita

Bajeti hiyo ina ongezeko la 13.2% zaidi ya ile ya mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo matarajio katika bajeti ya mwaka huu ni kugharamia na kuboresha miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia vipaumbele vilivyotajwa ikiwemo afya, miundombinu ya barabara pamoja na elimu kupitia ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Manispaa ya Geita  Ndg. Yefred Myenzi ameeleza namna walivyoweka mikakati ya kuboresha ukusanyaji wa mapato ili kuweza kufikia lengo sambamba na kunufaisha vikundi vyenye uhitaji.

Sauti ya mkurugenzi mtendaji Yefred Myenzi
Kaimu meya wa manispaa ya Geita Elias Ngole akizungumza na Storm FM. Picha na Ester Mabula

Kaimu meya ambaye pia ni diwani wa kata ya Nyanguku Elias Ngole ameeleza namna ambavyo bajeti hiyo imepambanua mahitaji ya msingi ya wananchi wa manispaa ya Geita.

Sauti ya Kaimu Meya Elias Ngole

Akizungumza kwa niaba ya madiwani, John Lunyaba Mapesa ambaye ni diwani wa kata ya Nyankumbu ameeleza matarajio yao mara baada ya kupitishwa kwa bajeti hiyo.

Sauti ya diwani wa kata ya Nyankumbu