Geita yazindua maonesho kuadhimisha wiki ya sheria
25 January 2025, 3:26 pm
Jumla ya mashauri 282 yalifunguliwa mwaka jana 2024 tangu kuanzishwa kwa mahakama kuu ya Tanzania masjala ndogo ya Geita.
Na: Kale Chongela – Geita
Jumla ya mashauri 282 yalifunguliwa mwaka jana 2024 tangu kuanzishwa kwa mahakama kuu ya Tanzania masjala ndogo ya Geita.
Hayo yamebainishwa na Jaji mfawidhi wa Mahakama kuu ya Geita Mhe. Kelvin David Mhina leo Januari 25, 2025 baada ya hafla fupi ya uzinduzi wa wiki ya sheria iliyofanyika katika viwanja wa EPZA eneo la Bombambili manispaa ya Geita ambapo amesema miongoni mwa mashauri yaliyowasilishwa ni pamoja na migogoro ya ardhi.
Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela ambaye alikuwa mgeni maalumu katika uzinduzi huo wa wiki ya sheria amewataka wananchi mkoani Geita kutumia vyema maonesho ya wiki ya sheria kwa kuwasilisha kero zao mbalimbali zinazohitaji ufafanuzi wa kisheria.
Ikumbukwe kuwa maadhimisho ya wiki ya sheria kwa mwaka 2025 inaongozwa na kauli mbiu isemayo: Tanzania ya 2050 Nafasi ya Taasisi zinazosimamia Haki ya madai katika kufika malengo makuu ya Dira ya Taifa ya maendeleo.