Storm FM

Dereva agonga nyumba 2 Mwabasabi na kutokomea

23 January 2025, 5:27 pm

Zoezi la kuondoa gari iliyogonga nyumba mbili. Picha na Kale Chongela

Gari dogo lenye namba za usajili T 205 DSV limegonga nyumba mbili katika mtaa wa Mwabasabi kata ya Nyankumbu manispa ya Geita.

Na: Kale Chongela – Geita

Ajali hiyo imetokea leo Januari 23, 2025 ambapo mmiliki wa nyumba mojawapo iliyoharibiwa katika ajali hiyo Bw. Johnson Simon amesema wakati tukio linatokea alikuwa karibu na nyumba yake na ndipo ghafla  gari hilo lilitokea kwa kasi na kupelekea ajali hiyo.

Sauti ya mmiliki wa nyumba

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamedai kusikitishwa na tukio hilo wakieleza kuwa ipo haja kwa madereva kupunguza mwendo kasi ili kupunguza ajali.

Sauti ya mashuhuda

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mwabasabi Bw. Juma Ramadhan Luge amekiri kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa baada ya dereva kusababisha tukio hilo alitokomea kusikojulikana na kwamba jitihada zinaendelea za kumtafuta ili aweze kulipa fidia kwa uharibifu uliofanyika.

Sauti ya mwenyekiti

Hata hivyo Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani lilifika eneo la tukio muda mfupi baada ya kupokea taarifa na kufanikiwa kuondoa gari hilo ambapo inaelezwa hakuna madhara yaliyompata binadamu isipokuwa uharibifu wa mali.

Gari dogo likiwa limetelekezwa na dereva baada ya ajali. Picha na Kale Chongela