Storm FM

Atuhumiwa kumlawiti mwanaume mwenzake Geita

23 January 2025, 12:22 pm

Mtuhumiwa (52) kushoto, kulia ni mlalamikaji (25) wakiwa katika ofisi ya serikali ya mtaa. Picha na Amon Mwakalobo

Licha ya serikali kukemea vitendo vya ukatili, bado matukio hayo yameendelea kujitokeza na kuacha maswali mengi kwa wananchi juu ya nini mwarobaini wa ukatili.

Na: Amon Mwakalobo – Geita

Kijana mmoja wa umri wa miaka 25 kutoka mtaa wa Msalala road manispaa ya Geita amemtuhumu mzee mmoja mwenye umri wa miaka 52 majina yao tumeyahifadhi, kwa kumuingilia kinyume na maumbile au kumlawiti wakiwa wamelala ambapo alikuwa mgeni wake.

Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jumatatu ya Januari 20, 2025 katika mtaa huo.

Kijana huyo amesema yeye ni mgeni hapa Geita na alikutana na mzee huyo sehemu ya kuuzia kitimoto wakafahamiana kuwa wanatoka mkoa mmoja wa Mara na ndipo siku alipokosa pa kulala siku ya jumapili akaomba ahifadhiwe na mzee huyo akakubali na kumfanyia ukatili huku huku kijana akiwa hajielewi.

Sauti ya kijana mlalamikaji

Kwa upande wake mzee huyo anayetuhumiwa amekana kuhusika na tukio hilo huku akimtaka kijana huyo akapimwe hospitali ili kujua ukweli.

Sauti ya mzee mtuhumiwa

Jirani wa mwanaume huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema ni kweli kijana huyo aliamka usiku wa manane akiwa analia na kuamsha majirani akisimulia mkasa huo.

Sauti ya jirani

Kwa upande wa mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Msalala Road Bw. Sostenes Kalist amekiri kupokea malalamiko hayo ofisini kwake na kumshauri kijana kupeleka malalamiko yake Polisi kwani yeye hana mamlaka ya kupatanisha kesi za aina hiyo.

Sauti ya mwenyekiti Sostenes Kalist