CCM yazindua jengo la kitega uchumi Jumuiya ya wazazi Geita
15 January 2025, 10:57 am
Watumishi wa Umoja wa Jumuiya wa wazazi kupitia chama cha mapinduzi (CCM mkoa wa Geita wametakiwa kutunza na Kulinda Nyumba za Jumuiya hiyo na wala wasigeuze Matumizi yake.
Na: Nicholaus Lyankando – Geita
Wakizungumza katika uzinduzi wa Jengo jipya la kitega uchumi la Jumuiya hiyo lililopo katika mtaa wa Magogo litakalo gharimu kiasi cha shilingi milioni 55, baadhi ya wenyeviti wa Jumuiya kutoka wilaya za Geita wameonya kuhusiana na matumizi mabaya ya nyumba hizo huku wakieleza mikakati ya kukamilisha maboma yaliyosalia.
Katibu wa Jumuiya wa wazazi mkoa wa Geita Bwana Philibet Ngemela ametaja thamani ya nyumba iliyokamilika ya katibu wa mkoa huku akieleza azma ya kuwa na majengo hayo ni pamoja na kuondokana na hali upangaji katika majengo ya watu binafsi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Geita Lukas Mazinzi amesema kufikia mwezi April mwaka huu watakuwa wamekamilisha maboma yote huku akitoa maagizo kwa wenyeviti wa wilaya kuwa waaminifu katika matumizi ya fedha za mradi.
Baada ya kukamilisha zoezi la uzinduzi nakuzitembelea Nyumba hizo za watumishi Jumuia hiyo walifanya Kikao cha kutathimini Shughuli zote zilizofanyika kutoka Mwaka jana hadi mwaka Huu