TARURA yachukizwa wanaoziba mitaro Geita
13 January 2025, 5:38 pm
Wakazi wa Geita wameelea kuhimizwa kutunza miundombinu ya barabara sambamba na kutoa taarifa pindi wanapobaini uharibifu wa miundombinu.
Na: Kale Chongela – Geita
Wakala wa barabara za mjini na vijijini TARURA wilaya ya Geita imekemea vikali tabia ya badhi ya wananchi kuziba mitaro kwaajili hali inayopelekea usumbufu na uharibifu wa miundombinu ya barabara.
Kaimu meneja wa TARURA wilaya ya Geita Mhandisi Cathbeth Robert akizungumza na Storm FM mapema leo Januari 13, 2025 akiwa ofisini kwake amesema amebaini changamoto hiyo baada ya kutembelea katika maeneo kadhaa mjini Geita.
Sanjari na hayo ameongeza kuwa ipo haja kwa kila mwananchi kuwa msitari wa mbele katika kulinda miundombinu ya barabara ikiwemo kutoa taarifa pindi anapobaini uharibifu wowote.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wakizungumza kwa nyakati tofauti walikiri juu ya uwepo wa changamoto hiyo.