Madereva bajaji wachangia damu kunusuru wagonjwa Geita
11 January 2025, 4:10 pm
Uhitaji ya damu salama umeendelea kusisitizwa kwa wananchi kujitokeza ili kujitolea kwaajili ya kuweza kunusuru wagonjwa wenye uhitaji wa damu salama.
Na: Edga Rwenduru – Geita
Madereva wa pikipiki zenye magurudumu matatu bajaji mkoa wa Geita wametakiwa kuwa na utamaduni wa kushiriki shughuli za kijamii kama kujitolea damu ili kushiriki katika jitihada za kuzuia vifo vya wagonjwa hospitalini wenye uhitaji wa damu salama.
Wakizungumza na Storm FM madereva hao Januari 10, 2025 katika egesho la hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita iliyopo eneo la Magogo ambao wameshiriki zoezi la kujitolea damu wamesema wameamua kufanya zoezi hilo ili kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji wa damu hususani wanaopata ajali za barabarani.
Joel Masala ni mwenyekiti wa egesho hilo ameeleza hapa namna walivyoanzisha utaratibu huo wa kuchangia damu kwa wagonjwa
Kwa upande wake Dkt. Emmanuel Mayo kutoka kitengo cha damu salama katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita amesema vijana hao ni mfano wa kuigwa kwani wameonesha thamani yao kwa kuchangia chupa 15 za damu.