Kocha mpya Geita Gold FC kuonekana kesho Januari 12, 2025
11 January 2025, 3:53 pm
Ligi ya NBC Championship inatarajiwa kuendelea kesho, ambapo wachimba dhahabu Geita Gold FC wanatarajiwa kuwa wenyeji wa Ccama la wana Stand United ya Shinyanga.
Na: Edga Rwenduru – Geita
Afisa habari wa klabu ya Geita Gold FC Samwel Dida amesema mchakato wa kupata kocha mpya wa kikosi hicho tayari umekamilika na kesho Januari 12, 2025 kocha huyo atakuwa uwanjani akitazama mechi.
Dida ameeleza hayo leo Januari 11, 2025 akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mkoani Geita kuelekea mchezo wa kesho muendelezo wa NBC championship kati ya Geita Gold FC dhidi ya Stand United ya mkoani Shinyanga utaopigwa majira ya saa 10 jioni katika dimba la Nyankumbu girls mjini Geita.
Aidha Dida amewataka mashabiki wa Geita Gold FC na wananchi wote kwa ujumla kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuona wachezaji wapya sita waliosajiliwa na kikosi hicho kupitia dirisha dogo la usajili.
Geita Gold watashuka dimbani kucheza na Stend United kwenye mwendelezo wa michuano ya NBC Chapionship huku kikosi kikiwa chini ya Choki Abeid kama kocha wa muda baada ya Amani Josiah aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi hicho kutimukia kwa wajerajera Tanzania prisons.