Storm FM

Wananchi wahimizwa kujiunga na mfuko wa NHIF

9 January 2025, 10:38 am

Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Geita Elius Odhiambo akiwa katika studio za Storm FM

Kwa sasa kuna mabadiliko ya vifurushi vya matibabu kupitia mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) ambavyo vinaendelea kutoa fursa kwa wananchi kupata matibabu.

Na: Paul William – Geita

Wananchi mkoani Geita wametakiwa kujiunga na mfuko wa Taifa wa bima ya afya ili kuwa na uhakika wa kupata huduma za kimatibabu pindi wanapopata changamoto za kiafya kwani ugonjwa huja bila taarifa.

Wito huo umetolewa na meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) mkoa wa Geita Elias Odhiambo alipokuwa akifanya mahojiano kupitia kipindi cha Storm Asubuhi mapema Januari 08, 2025.

Sauti ya meneja NHIF Geita

Kwa upande wa wanafunzi Bw. Odhiambo amezitaka shule za UMMA, binafsi na vyuo kukamilisha utaratibu wa kusajili wanafunzi kupitia utaratibu wa bima ya afya kwa wanafunzi kwani itasaidia kuwa na uhakika wa matibabu kwa wanafunzi.

Sauti ya meneja NHIF Geita

Ameongeza kuwa bima hiyo inatumika mwanafunzi awapo shuleni au hata anapokuwa nje ya shule bado ataweza kutumia kadi yake ya matibabu.