TANROADS yaanza maboresho barabara ya Geita mjini – Nzera
3 January 2025, 9:46 am
Kufuatia changamoto ya ubovu wa miundombinu ya barabara katika baadhi ya maeneo mjini Geita, hatimaye marekebisho ya baadhi ya barabara hizo yameanza kutekelezwa.
Na: Kale Chongela – Geita
Wakala wa barabara nchini TANROADS mkoa wa Geita yaanza kufanya maboresho na matengenezo ya barabara kutoka Geita mjini hadi Nzera kwa urefu wa KM 26 kwa kiwango cha moramu.
Akizungumza na Storm FM mkuu wa kitengo cha matengenezo wa TANROADS mkoa wa Geita mhandisi Fredrick Mande Januari 02, 2024 akiwa eneo la Lukirini amesema matengenezo hayo yanatarajiwa kukamilika mwezi wa sita mwaka 2025 na kwamba matengenezo hayo yanatekelezwa na mkandarasi Soro Company Limited.
Aidha ameongeza kwa kuwasihi madereva wa vyombo vya moto wanaotumia barabara hiyo kuendesha kwa uangalifu kwani ipo mitambao ambayo ipo barabara inaendelea kutekeleza matengezo hayo.
Baadhi ya watumiaji wa barabara hiyo hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti wameiopongeza serikali kwa hatua hiyo huku ombi lao wakiomba serikali kuiweka katika mfumo wa lami.