Waandishi watakiwa kutokuwa sababu ya migogoro Geita
20 December 2024, 6:56 pm
Kutokana na umuhimu wa tasnia ya habari kuwa nyeti , waandishi wameendelea kusisitizwa kufanya kazi zao kwa weledi kwakuwa jamii inawategemea.
Na Mrisho Sadick:
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Geita Renatus Masuguliko amewataka waandishi wa habari mkoani humo kutokuwa sehemu ya migogoro ikiwemo kutisha watu katika jamii nabadala yake wafanye kazi zao kwa kufuata misingi ya taaluma hiyo.
Masuguliko ametoa kauli hiyo Disemba 12,2024 kwenye Mkutano mkuu wa mwaka wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Geita uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa bwalo la Polisi mjini Geita ambapo amewataka waandishi wa habari kujiepusha na mambo yasiyofaa katika jamii.
Makamu mwenyekiti wa GPC Victor Barriety ametumia nafasi hiyo kuwasisitiza waandishi wa habari kujikita kuandika habari zenye manufaa kwa jamii nakuzingatia ulinzi na usalama wao binafisi kwakuwa jukumu hilo linaanza na wao.
Baadhi ya waandishi wa Habari walioshiriki katika Mkutano huo Editha Edward , Elias Zephania na Marco Kanani wameahidi kuendelea kufanya kazi zao kwa kuzingatia misingi ya taaluma yao kwakuwa jamii inatambua mchango wao.