CCM yalaani mtoto kuchomwa moto Kasota
13 December 2024, 1:57 pm
Kufuatia tukio la mtoto Disemba 02, 2024 la mtoto kushambuliwa na kuchomwa moto na mama yake mzazi likatika kijiji cha Kasota wilayani na mkoani Geita, CCM mkoa wa Geita yalaani tukio hilo.
Na: Evance Mlyakado – Geita
Jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Geita imelaani vikali tukio la mtoto mwenye umri wa miaka (9) kushambuliwa na kuchomwa moto kwa mafuta ya petrol na mama yake mzazi kwa madai ya kuiba shilingi 800 katika kijiji cha Kasota wilayani Geita.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoa wa Geita Lucas Mazinzi akiwa kwenye kikao cha baraza la jumuiya ya wazazi wilayani Nyangh’wale amesema amepanga kuzunguka mkoa mzima wa Geita kukutana na viongozi, wananchi na kamati za utekelezaji ili kuweka mikakati ya kukomesha vitendo vya ukatili
Mwenyekiti wa CCM wilayani Nyang’hwale Al haj Adam Mtole amesema kuwa CCM haitawafumbia macho watu wote wanaondelea kufanya vitendo vya ukatili katika jamii.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita SACP Safia Jongo alithibitisha kukamatwa kwa mwanamke huyo na kwamba taratibu za uchunguzi zaidi zinaendelea.