Storm FM

Wafanyabiashara soko la Lwamgasa watoa ombi kwa Serikali

13 December 2024, 12:04 pm

Shughuli mbalimbali zikiendelea katika soko la Lwamgasa ambapo wateja mbalimbali wanaendelea na ununuzi wa bidhaa. Picha na Paul William

Lwamgasa ni miongoni mwa kata 37 zilizopo katika halmashauri ya wilaya ya Geita ambapo shughuli kuu inayofanyika katika kata hiyo ni uchimbaji wa madini ya dhahabu.

Na: Paul William – Geita

Wafanyabiashara mbalimbali katika soko kuu la kata ya Lwamgasa wilayani na mkoani Geita wameiomba serikali kuwasaidia kuboresha soko hilo kutokana na kuzidiwa na idadi ya watu wanaofika hapo kwaajili ya kupata huduma

Wakizungumza na Storm FM Disemba 13, 2024 wamesema endapo soko hilo litaboreshwa itasaidia kuweza kuongeza mapato na kutoa wigo mpana kwa wao kufanya biashara pasipo kulundikana kwani kwa sasa linazidiwa na watu.

Sauti ya wafanyabiashara
Muonekano wa baadhi ya maeneo katika soko la Lwamgasa lililopo wilayani Geita. Picha na Paul William

Akizungumzia suala hilo mjumbe wa serikali ya mtaa Bwana Fredrick Jeremia Wambowe amesema kwa kuwa wamechaguliwa na wananchi katika kitongoji hicho ambapo soko hilo linapatikana watahakikisha soko hilo linaboreshwa.

Sauti ya mjumbe

Wakingumzia hali ya kibiashara katika soko hilo kwa sasa katika msimu huu wa mwisho wa mwaka, wafanyabiashara wamesema hali ya kimauzo inabadilika badilika.

Harakati na shughuli mbalimbali za manunuzi zikiendelea katika soko la Lwamgasa. Picha na Paul William