Storm FM

DC Geita atoa maelekezo ya utendaji kwa wenyeviti

6 December 2024, 4:54 pm

Mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba akizungumza na wenyeviti (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika eneo la EPZA. Picha na Ester Mabula

Mkuu wa wilaya ya Geita ametoa mwongozo wa kiutendaji kwa wenyeviti kutoka kata 13 za halmashauri ya mji wa Geita na kata 37 za halmashauri ya wilaya ya Geita.

Na: Ester Mabula – Geita

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba amewasisitiza wenyeviti waliochaguliwa kuzingatia miiko ya kiutendaji na kufanya kazi kwa maslahi ya wananchi ili kuchochea maendeleo katika maeneo yao.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika Disemba 05, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa EPZA katika halmashauri ya mji wa Geita Mhe. Komba amewasisitiza kutatua kero za wananchi na kuepuka migongano na wananchi wao.

Sauti ya DC Geita
Katibu mwenezi na mafunzo wa CCM wilaya ya Geita Gabriel Nyasilu akizungumza na wenyeviti (hawapo pichani). Picha na Ester Mabula

Akizungumza katika mkutano huo Katibu mwenezi na mafunzo wa CCM wilaya ya Geita Gabriel Nyasilu amewaeleza wenyeviti kufanya kazi kwa bidii ili kuendeleza imani ya Chama kwani imewaamini na kuwapa ridhaa kuweza kusaidia wananchi

Sauti ya katibu mwenezi CCM

Baadhi ya wenyeviti wakizungumza baada ya mkutano huo wameeleza namna walivyopokea maelekezo ya mkuu wa wilaya na kuahidi kuyafanyia kazi

Sauti ya wenyeviti
Wenyeviti wa mitaa, vijiji na vitongoji wakiwa katika mkutano wa kupewa maelekezo na mkuu wa wilaya ya Geita. Picha na Ester Mabula

Uchaguzi wa serikali za mitaa ulifanyika Novemba 27, 2024 ambao uluhusisha uchaguzi wa wenyeviti wa mitaa, vitongoji na vijiji katika mikoa ya Tanzania bara.