Storm FM

Wazazi walaani tukio la mtoto kuchomwa moto Kasota

5 December 2024, 12:49 pm

Muonekano wa baadhi ya sehemu za halmashauri ya mji wa Geita. Picha kwa msaada wa Google.

Matukio ya ukatili kwa watoto bado ni pasua kichwa, jamii yatakiwa kushikamana ili kukomesha kabisa vitendo hivyo.

Na: Sammy Manilaho – Geita

Wakazi wa halmashauri ya mji wa Geita wamelaani vikali tukio la mama kumchoma moto mtoto wake kwa kutumia mafuta ya petrol kwa madai ya kuiba shilingi 800 katika kijiji cha Kasota kata ya Bugulula halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani Geita.

Wakizungumza na Storm FM kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa mji wa Geita wameishauri jamii na serikali kuwa macho kutokana kuongezeka kwa vitendo vya ukatili hususani kwa watoto ambavyo vinafanywa hadi na wazazi jambao ambalo linahitaji nguvu ya ziada kuvidhibiti.

Sauti ya wakazi wa mji wa Geita

Tukio hilo lilitokea Disemba 02, 2024 baada ya mama mzazi wa mtoto huyo wa miaka tisa anaesoma darasa la tatu katika shule ya msingi kasota kudaiwa kuiba shilingi 800 kisha kupewa adhabu ikiwemo vipigo nakisha kuchomwa moto nakumjeruhi sehemu ya shingo, kifuani na mikononi.

Baada ya tukio hilo kutokea mtoto huyo alikimbizwa katika kituo cha afya Kasota na hali yake ilivyozidi kuwa mbaya alikimbizwa katika Hospitali ya Nzera kwa matibabu zaidi , kamanda wa polisi mkoa wa Geita Safia Jongo alithibitisha kukamatwa kwa mwanamke huyo na taratibu za kipolisi zikikamilika atafikishwa mahakamani.