Storm FM

Wakulima wageuka mbogo Geita

5 December 2024, 12:27 pm

Wakulima wakiwa katika mashamba yao kuimarisha ulinzi.Picha na Kale Chongela

Serikali imetakiwa kutatua migogoro mapema kabla ya watu kuanza kujichukulia sheria mkononi hali ambayo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Na Kale Chongela:

Wakulima wa Kata ya Bombambili halmashauri ya mji wa Geita Mkoani Geita wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kuwazuia baadhi ya wafugaji wanaoendelea kuingiza mifugo kwenye mashamba yao ili kuepuka kukua kwa mgogoro huo unaoweza kusababisha mauaji.

Wakulima hao Aloyse Kulwa na Lusia Mapato wakiwa kwenye mashamba yao wamedai baadhi ya wafugaji wa Ng’ombe katika eneo hilo wamekuwa na tabia ya kuingiza mifugo kwenye mashamba yao nyakati za usiku kulisha nakufanya uharibifu wa mazao yao.  

Sauti za wakulima
Miongoni mwa mifugo inayodaiwa kulisha kwenye mazao ya wakulima. Picha na Kale Chongela

Katika hatua nyingine wakulima hao Dickson Gabriel na Khamis Bitara wamesema baadhi ya wafugaji bila kuwataja majina yao wamekuwa wakiwatisha huku wakiiomba serikali kuingilia kati mgogoro huo haraka ili kuepuka uvunjifu wa amani.

Sauti za wakulima

Afisa kilimo , mifugo na uvuvi wa halmashauri ya mji wa Geita Leonard Chacha amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo nakwamba ameshatuma wataalamu kwenda katika eneo hilo kutatua mgogoro.