Storm FM

Vikundi 81 vyanufaika na mikopo ya 10% mjini Geita

26 November 2024, 4:43 pm

Afisa maendeleo halmashauri ya mji wa Geita Valeria Makonda akizungumza na wajasiriamali waliojitokeza kwaa ajili ya mikopo ya 10%. Picha na Kale Chongela

Mikopo ya asilimia 10 ambayo imeendelea kutolewa na serikali ya Tanzania imeendelea kunufaisha watu mbalimbali katika makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kupitia miradi mbalimbali wanayoifanya.

Na: Kale Chongela – Geita

Jumla ya vikundi 81 kutoka katika kata 13 za halmashauri ya mji wa Geita wameaanza kunufaika na mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na halmashauri ili wajikwamue kiuchumi.

Hayo yameelezwa na mkuu wa wilaya ya Geita Mhe. Hashim Komba Novemba 25, 2024 akiwa katika ukumbi wa mikutano wa GEDECO  mjini Geita wakati akizungumza na  wajasiriamali ambao ndiyo wanufaika wa mikopo hiyo.

Sauti ya DC Geita

Mkurugenzi  wa halmashauri ya mji wa Geita Yefred Myenzi amesema kwa sasa kuna maboresho ambayo yamefanyika katika kuhakikisha wananchi wa mji wa Geita wananufaika na fedha hizo ikiwa ni pamoja na kuongeza umri wa wanufaika hadi umri wa miaka 45.

Sauti ya mkurugenzi Geita mjini
Wajasiriamali wakiwemo vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ambao ni wanufaika wa mikopo ya asilimia kumi. Picha na Kale Chongela

Baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo wametumia fursa hiyo kuishukuru serikali ya awamu sita kwa kuendelea kuwawezesha na kuwapa fursa za kujikwamua zaidi kiuchumi.

Sauti ya wajasiriamali