Storm FM

Jaketi chafu la dereva pikipiki egesho la Mpomvu lachomwa moto

14 November 2024, 10:16 am

Jaketi la dereva pikipiki likiteketea kwa moto baada ya kuchomwa na wanachama wenzake. Picha na Kale Chongela

Madereva pikipiki mkoa wa Geita wameendelea kusisitizwa kuzingatia usafi hali ambayo inapelekea baadhi ya maegesho kuweka sheria ndogo ndogo ili kuzingatia hilo.

Na: Kale Chongela – Geita

Madereva pikipiki waliopo katika egesho la Mpomvu A kata ya Mtakuja halmashauri ya mji wa Geita wamechoma jaketi la dereva mwenzao ambaye ni mwanachama wa egesho hilo kwa kile walichoeleza kuwa lilikuwa chafu kupitiliza.

Storm Fm ilifika katika mtaa huo kwaajili ya kujiridhisha juu ya kile kilichotokea  ambapo yalizuka majibizano kutokana na hatua hiyo iliyochukuliwa.

Sauti ya majibizano ya madereva

Baada ya majibizano hayo, baadhi ya wanachama wameeleza sababu hasa zilizopolekea kuchukua uamuzi huo wa kuchoma moto jaketi.

Sauti ya wanachama
Muonekano wa Jaketi la dereva pikipiki kabla ya kuchomwa moto na wanachama wenzake. Picha na Kale Chongela

Mwenyekiti wa egesho hilo Bw. Lenard Masele amesema licha ya kuweka makubaliano juu ya usafi pamekuwepo na hali ya baadhi ya wanachama kupuuza agizo hilo na kwamba wameanza kusimamia utaratibu ambao waliuweka katika egesho hilo.

Sauti ya mwenyekiti wa egesho

Mwenyekiti wa kata ya Mtakuja Bw Yohana mathias amebainisha kuwa  mtumiaji wa jaketi hilo aliwahi kulalamikiwa na abiria kuwa jaketi hilo limekuwa chafu hali ambayo ilikuwa ikisababishwa kutoa harufu mbaya kwa wateja.

Sauti ya mwenyekiti kata ya Mtakuja
Wanachama wa egesho la pikipiki mtaa wa Mpomvu A baada ya kuchoma Jaketi la mwanachama mwenzao. Picha na Kale Chongela