Storm FM

Wananchi 226 walipwa fidia wilayani Nyang’hwale

12 November 2024, 3:28 pm

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Geita Azza Mtaita akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Picha na Kale Chongela

Jumla ya wananchi 226 katika kata ya Mwingiro  wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita wamelipwa fidia ya zaidi ya shilingi bilioni 7.2  kutokana na maeneo yao kuchukuliwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa zaidi ya miaka 20 .

Na: Kale Chongela – Geita

Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Geita  Bw. Azza Mtaita akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 12, 2024 amesema maeneo hayo ya wanachi yalichukuliwa na mgodi huo kwa zaidi ya miaka 20 bila  wananchi kunufaika  chochote  ndipo TAKUKURU  wakaanza kufanya ufuatiliaji.

Sauti ya mkuu TAKUKURU
Muonekano wa nje wa jengo la ofisi za TAKUKURU mkoa wa Geita. Picha na Kale Chongela

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2024 jumla ya kesi 15 zinazohusu Rushwa ziliendelea katika mahakama mbalimbali ndani ya mkoa wa Geita.

Sauti ya mkuu TAKUKURU

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa TAKUKURU imejipanga kuendelea kudhibiti vitendo vya Rushwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.

Sauti ya mkuu TAKUKURU