Storm FM

CHADEMA waeleza kubaini udanganyifu zoezi la uandikishaji Geita mjini

25 October 2024, 1:58 am

Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) jimbo la Geita Pasquiner Ferdinand. Picha na Edga Rwenduru

Leo ni siku tano tangu kukamilika kwa zoezi la uandikishaji katika daftari la makazi kwaajili ya mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji unaotarajia kufanyika Novemba 27, 2024.

Na: Edga Rwenduru – Geita

Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mkoani Geita kimedai kubaini udanganyifu katika zoezi la uandikishaji wa wapiga kura katika daftari la makazi katika kata za Kasamwa, Kanyala na Mtakuja zilizopo halmashauri ya mji Geita ambapo watendaji wa serikali wanadaiwa kuandika majina hewa katika daftari la wakazi.

Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Geita Pasquiner Ferdinand amesema katika mtaa wa NMC mtu wa mwisho kuandikwa alikuwa namba 647 siku ya Oktoba 20, 2024 ambayo ilikuwa siku ya mwisho ya zoezi hilo lakini wamegundua kuwa majina hewa zaidi ya 300 yameongezwa.

Sauti ya mwenyekiti CHADEMA

Pius Magembe ambaye alikuwa wakala wa CHADEMA katika kituo cha NMC amebainisha kuwa majina yaliyoongezwa yanakinzana tarehe ya kumalizika kwa zoezi hilo.

Sauti ya wakala CHADEMA
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita Barnabas Mapande akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Edga Rwenduru

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita Barnabas Mapande amesema zoezi la uandikishaji limeenda vizuri bila shida yoyote.

Sauti ya mwenyekiti CCM
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Geita mjini Yefred Edson Myenzi akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake. Picha na Edga Rwenduru

Naye msimamizi wa uchaguzi jimbo la Geita mjini ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji Geita Yefred Myenzi amesema hadi sasa hajapokea malalamiko yoyote na kwamba zoezi limeendeshwa kwa mujibu wa kanuni na miongozo iliyowekwa.

Sauti ya msimamizi wa uchaguzi