Storm FM

UVCCM Geita yaonya madai ya vijana kutishwa

20 October 2024, 8:20 pm

Baadhi ya wanachama wa CCM wakiwa katika mkutano wa mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Geita. Picha na Mrisho Sadick

Joto la uchaguzi wa serikali za mitaa limeendelea kupanda kila kukicha huku vijana wakianza kuona dalili za kukatishwa tamaa kuwania nafasi za uongozi.

Na Mrisho Sadick:

Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Geita umekemea vikali madai ya uwepo wa baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa  wanaomaliza muda wao kuwatisha vijana wanao onesha nia ya kugombea  nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Geita Manjale Magambo wakati akizungumza na wanachama wa chama hicho mtaa wa mbugani Halmashauri ya mji wa Geita ambapo amesema tayari chama hicho kimepokea taarifa ya baadhi ya vijana wanao onesha nia ya kugombea katika uchaguzi wa serikali za mitaa kutishwa ili wasichukue fomu muda utakapo wadia.

Sauti ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Geita
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Geita akizungumza na wanachama wa CCM Mtaa wa Mbugani mjini Geita. Picha na Mrisho Sadick

Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Geita Gabriel Nyasilu amesema chama hicho kimelelewa katika misingi ya demokrasi huku akiwataka watu wote wenye sifa kwenda kuchukua fomu.

Hali hiyo inakuja ikiwa uongozi wa wenyeviti wa serikali za mitaa nchini kukoma tangu oktoba 19,2024 ili kuruhusu taratibu zingine za kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa novemba 27 ziweze kuendelea  kuendelea.

Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Geita akizungumza na wanachama wa CCM Mtaa wa Mbugani mjini Geita. Picha na Mrisho Sadick