Storm FM

TANROADS yatatua kero ya barabara Nyantorotor A

16 October 2024, 9:43 am

Muonekano wa barabara ambayo imefanyiwa marekebisho na TANROADS mtaa wa Nyantorotoro A. Picha na Kale Chongela

Wakala wa barabara nchini Tanzania (TANROADS) wasaidia katika utatuzi wa barabara ya Nyantororo A ambayo ilikuwa changamoto kwa wakazi wa eneo hilo.

Na: Kale Chongela – Geita

Kufuatia uwepo wa changamoto ya baadhi ya madereva wa vyombo vya moto kutumia njia ya mchepuo katika mtaa wa Nyantorotoro A kata ya Nyankumbu halmashauri ya mji wa Geita, hatimaye TANROADS wamefanya marekebisho wa eneo hilo.

Oktoba 14, 2024 Storm FM imefika katika eneo hilo ambapo baadhi ya wananchi wameleza kuwa baada ya kuwekwa matuta imesaidia kuondoa changamoto.

Sauti ya wananchi

Mtaalamu kutoka wakala wa barabara TANROADS mkoa wa Geita mhandisi Fedrick Mande akizungumza kwa njia ya simu amesema dhamira ya serikali ya awamu ya sita ni kutatua changamoto ambazo ni kikwazo kwa wananchi na kwamba wanaendelea kufanya maboaresho kwenye maeneo korofi ya barabara.

Sauti ya mhandisi