Storm FM

Wananchi wahofia kupita daraja la Katundu nyakati za usiku

7 October 2024, 9:52 am

Muonekano wa daraja la Katundu ambalo linatumiwa na wananchi kupita. Picha na Amon Mwakalobo

Uwepo wa daraja la Katundu ambalo linatumiwa na wananchi mbalimbali umepelekea hofu kwa baadhi ya wananchi kutokana na baadhi ya vijana kukaa hasa nyakati za usiku.

Na: Amon Mwakalobo – Geita

Baadhi ya wananchi halmashauri ya mji wa Geita wanaoutumia barabara ya Jimboni kupitia mtaa wa Katundu wameuomba uongozi wa mtaa wa Katundu kuhakikisha wanakomesha tabia ya baadhi ya vijana kukaa kwenye katika daraja lilipo mtaani hapo huku wakiwa hawana kazi ya kufanya hasa nyakati za usiku.

Wakizungumza na Storm FM Oktoba 05, 2024 wamesema wamekuwa wakiogopa kupita maeneo hayo kwa uhuru kwani vijana hao wamekuwa wanakaa kwa vikundi na wanaonekana kama ni vibaka.

Sauti ya wananchi

Kwa upande wa baadhi ya wanawake nao wamesema imekuwa ngumu kwao kupita katikati ya kundi la wanaume hasa usiku hivyo kuna wakati inawalazimu kurudi na kutafuta njia nyingine ya kuoita kuelekea makwao.

Sauti ya wanawake

Kamanda wa polisi jamii mtaa huo Alfan Boniphace amekiri kuwepo kwa vijana wa aina hiyo na kueleza hatua wanazoendelea kuchukua.

Sauti ya kamanda

Mwenyekiti wa mtaa huoGidion Ally ameahidi kulishughulikia suala hilo haraka iwezekanavyo.

Sauti ya mwenyekiti