Kiongozi mbio za mwenge aridhishwa na mradi wa maji Mbogwe
3 October 2024, 9:43 am
Mwenge wa uhuru umeendelea kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Geita tangu ulipokabidhiwa rasmi Septemba 30, 2024.
Na: Kale Chongela – Geita
Mbio za Mwenge wa uhuru zimeridhishwa na mradi wa maji wenye thamani ya 2,050,923,546.11 uliopo wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
Akitoa taarifa mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Oktoba 02, 2024 mhandisi wa wakala wa maji vijijini (RUWASA) wilaya ya Mbogwe Mhandisi Rodrick Mbepera amesema mradi huo unatarajia kukamilika mwezi April, 2025.
Baadhi ya wananchi wa eneo hilo wameishukuru serikali kwa ujenzi wa mradi huo wa maji kwani utawasaidia kuondoa changamoto ya muda mrefu kutokana na kusogezewa karibu huduma ya maji.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa Ndugu Godfrey Mzava ameweka njiwe la msingi katika mradi huo wa maji wenye tenki la ujazo wa lita laki moja na elfu hamisini.