Storm FM

Katibu mkuu ACT Wazalendo ahitimisha ziara mkoani Geita

2 October 2024, 10:55 am

Katibu mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu Ado akizungumza na wananchi wa Runzewe wilayani Bukombe mkoani Geita.

Ziara ya katibu mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu katika maeneo mbalimbali mkoani Geita imetamatika kwa kutembelea halmashauri ya wilaya ya Bukombe.

Na: Ester Mabula – Geita

Katibu mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu Ado Septemba 30, 2024 amehitimisha ziara yake mkoani Geita kwa kuzungumza na wananchi na wakazi wa Runzewe wilaya ya Bukombe.

Baadhi ya wakazi wa Runzewe wilayani Bukombe wakimsikiliza katibu mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu Ado.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara ameeleza wakazi wa Bukombe na maeneo ya Geita kwa ujumla wanategemea kilimo kwaajili ya kujikwamua kimaisha na kuongeza pato la taifa, amesisitiza serikali kuweka mazingira rafiki kwa wakulima ili waweze kupata manufaa.

Sauti ya katibu mkuu ACT Wazalendo
Baadhi ya wakazi wa Runzewe wilayani Bukombe wakiwa katika mkutano wa hadhara wa katibu mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu Ado.

Akizungumzia changamoto za wafanyabiashara wa Runzewe amesema wamekuwa wakipitia changamoto ikiwemo tozo na kodi pamoja na umiliki wa ardhi katika maeneo yao ya biashara.

Sauti ya Katibu mkuu ACT Wazalendo

Ziara ya Katibu mkuu wa ACT Wazalendo kwa mikoa ya kanda ya ziwa ilianza Septemba 20, 2024 ambapo ametembelea mikoa ya Simiyu, Mara, Mwanza, Geita na itamalizikia mkoani Kagera.

Baadhi ya wakazi wa Runzewe wilayani Bukombe wakiwa katika mkutano wa hadhara wa katibu mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu Ado.