Storm FM

Anastazia aliyevunjika mgongo bado anaomba msaada

24 September 2024, 7:26 pm

Muonekano wa picha za Anastazia akiwa jijini Mwanza katika harakati za kupambania afya yake baada ya kuvunjika uti wa mgongo. Picha na Mrisho Sadick

Mkazi wa Geita na Tanzania tuungane kwa mara nyingine tena kuendelea kumsaidia Anastazia kwakuwa pesa ulizojitoa kumchangia nakupata nafasi ya kupata matibabu katika Hosptali ya Bungando Jijini Mwanza zimeisha namba ya msaada ni 0756397026.

Na Mrisho Sadick:

Siku zote hatuwezi kuacha kuishi katika maneno na misemo mbalimbali ya wahenga ambapo kuna wakati walisema umoja ni nguvu utengano ni udhaifu na kidole kimoja hakivunji chawa.

kauli hizi zimethibitishwa na wananchi wa Geita na Tanzania kwa ujumla kwa kujitoa sehemu ya kipato chao kwa ajili ya kumsaidia Anastazia Jackob mwenye umri wa miaka (22) kutoka mtaa wa mabamba kijiji cha Inyala kata ya Nyamigota wilayani Geita aliyevunjika uti wa mgongo baada ya kuanguka kutoka juu ya mti wa mwembe nakukaa ndani kwa zaidi ya miaka 2 bila usaidizi wowote.

Muonekano wa Anastazia aliyekuwa hawezi hata kujiinua kwa miaka miwili akiwa Hosptal ya Bugando jijini mwanza kwasasa mambo yanaendelea kuwa vizuri. Picha na Mrisho Sadick

Jitihada za wadau wenye moyo wa huruma kwa kuongozwa na kituo cha Redio cha Storm FM zimemuwezesha mwanamke huyu kufikishwa katika Hosptal ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza kwa ajili ya matibabu lakini licha ya kupatiwa matibabu kwa zaidi ya miezi miwili hali yake bado haijatengamaa kutokana na huduma anazotakiwa kupatiwa kuwa na gharama kubwa nakwasasa pesa yote iliyochangwa na wadau imeisha.

Sauti ya Anastazia Jackobo

Akizungumza na Storm FM Jijini Mwanza Anastazia ameeleza matibabu yote anayotakiwa kupatiwa katika Hosptali ya Rufaa ya Bugando ili aweze kurudi katika hali yake ya kawaida , kutokana na ukata wa fedha ametumia nafasi hii kukuomba wewe mtanzania kuendelea kumsaidia kwa mara nyingine kwani nguvu yako wewe uliyejitoa kwa mara ya kwanza imeonekana kuleta matumaini.

Sauti ya Anastazia Jackobo

NAMBA YA KUTUMA MCHANGO WAKO NI – 0756397026 JINA NI ESTER MABULA: