Storm FM

Binti akataa kuolewa baada ya kulazimishwa na wazazi

12 September 2024, 8:07 pm

Picha ya binti aliyekataa kuolewa baada ya kulazimishwa na mama yake mzazi. Picha na Kale Chongela

Akataa kuolewa baada ya mama mzazi kudaiwa kumlazimisha aolewe kwa nguvu , mama mzazi akanusha tuhuma hizo.

Na kale chongela:

Msichana mwenye umri wa miaka 18 mkazi wa mtaa wa Mpomvu kata ya Mtakuja Halmashauri ya mji wa Geita Mkoani Geita ambaye jina lake limehifadhiwa amekata kuolewa baada ya kulazimishwa na mama yake mzazi.

Sauti ya binti 1

Septemba 12 Storm FM imefika katika mtaa huo ambapo binti huyo amesema mnamo tarehe 9 ya mwezi wa 9 Mama yake mzazi aliweka mazingira kwa kijana huyo ambaye yeye alimtaka awe mkwilima wake ndipo binti huyo alipelekwa hadi nyumbani kwa kijana huyo  baada ya kuambia kuwa kijana huyo atakuwa mume wake ndipo  mzozo ukaanza .

Sauti ya binti 2

Bi Kefrine Stephano ni mama mzazi wa binti  akizungumza akiwa katika eneo ambapo anafanyia kazi yake ya kujiingizia kipato ya kutoa huduma ya chakula katika eneo la Njia Panda ya Nyarugusu amekanusha taarifa hiyo na kueleza kuwa wao wenyewe walikubaliana  kuwa wataoana.

Sauti ya mama mzazi wa binti

Balozi wa eneo hilo Bw Amos John amesema baada ya kupokea taarifa hiyo  anatarajia kuwaita  wahusika wote  kijana ,mama mzazi na Binti ambaye amelazimisha kuolewa ili suala hilo litatuliwe ikiwemo wahusika

Sauti ya balozi wa eneo hilo.

Balozi wa Mponvu akizungumza na Storm FM kuhusu tukio hili. Picha na Kale Chongela