Walimu wa MEMKWA Geita waomba vifaa
6 September 2024, 4:32 pm
Serikali imeendelea kutoa fursa za watoto pamoja na watu wazima kujiendeleza kimasomo kupitia mipango ya MEMKWA, SEQUIP na MUKEJA ili kuweza kuwasaidia kupata ujuzi.
Na: Edga Rwenduru – Geita
Walimu wanaofundisha elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi mkoani Geita wameiomba serikali kuwaletea vitendea kazi vya kutosha pamoja na kuwaboreshea mazingira ya ufanyaji kazi.
Wakizungumza wakati wa maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima kimkoa iliyofanyika wilaya ya Bukombe Septemba 05, 2024 wamesema changamoto ya ukosefu wa vitendea kazi vya kutosha na mazingira yasiyo rafiki imekuwa kikwazo.
Justus Mtachoka na Juma Ibrahimu wakizungumza kwa niaba ya walimu wengine wamefafanua juu ya changamoto hizo.
Licha ya mkoa wa Geita kuwa na walimu 199 wanaofundisha elimu ya watu wazima lakini bado changamoto kutotengewa bajeti kwaajili ya elimu hiyo imeendelea kuwepo.
Mkuu wilaya ya Mbongwe Sakina Mohammed kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Geita ameagiaza halmashauri zote za mkoa wa Geita kutenga bajeti kwaajili ya elimu ya watu wazima .