Storm FM

Wananchi wakerwa kusuasua ujenzi wa barabara

5 September 2024, 3:42 pm

Muonekano wa barabara ambayo inafanyiwa marekebisho. Picha na Kale Chongela

Kusuasua kwa ujenzi wa barabara yenye urefu wa mita 600 mkabala na kituo kikubwa cha magari ya abiria mjini Geita hadi soko la Mbagala kunatajwa kuongeza changamoto.

Na: Kale Chongela – Geita

Akizungumza kwa niaba ya madereva wenzake ambao hutumia barabara hiyo wameiambia Thobias Magwina amesema kuwa kasi ya ujenzi wa barabara hiyo imepungua tofauti na mwanzo na hivyo inawapa wasiwasi juu ya mradi huo huenda usikamilike kwa wakati.

Sauti ya dereva

Hata hivyo  wananchi wa eneo hilo wametumia fursa hiyo kuuomba uongozi wa  wakala wa barabara Mkoa wa Geita ambao ndio wasimamizi wa barabara hiyo TANROADS  kumhizi mkandarasi ili waweze kuondokana na changamoto iliyopo kwa sasa.

Sauti ya wananchi

Msimamizi wa barabara hiyo kutoka TANROADS mkoa wa  Geita mhandisi Joram John amesema barabara hiyo inatekelezwa na kampuni ya Josam Engineering Company Limited na kwamba mradi huo unatakiwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu 2024 kwa mujibu wa mkataba.

Sauti ya mhandisi