Storm FM

Mtoto (6) afariki bwawani akivua samaki Lulembela

2 September 2024, 11:36 am

Bwawa ambalo limeondoa uhai wa Rashid Paul. Picha na Evance Mlyakado

Uhai wa mtoto Rashid Paul wakatishwa baada ya kuzama kwenye bwawa la maji ya umwagiliaji na kunyweshea mifugo

Na Evance Mlyakado- Geita

Mtoto wa kiume Rashid Paul John mwenye umri wa miaka 6 katika kitongoji cha Ilyamchele, kijiji cha Kabanga Kata ya Lulembela wilaya ya Mbogwe mkoani Geita amefariki dunia baada ya kuzama katika Bwawa la maji lililochimbwa kwa ajili ya shughuli za kilimo cha umwagiliaji.

Tukio hilo limetokea Ijumaa ya Agosti 30,2024 ambapo marehemu Rashid Paulo akiwa na mtoto mwenzake mwenye umri sawa na wake wakichunga mbuzi alifikwa na umauti baada ya kuzama kwenye bwawa hilo wakati akivua samaki.

Sauti ya baba mzazi wa Rashid
Paul John baba mzazi wa Rashid Paul akizungumzia tukio la mtoto wake kufariki. Picha na Evance Mlyakado

Kwa upande wake baadhi ya wakazi wa kijiji hicho akiwemo Simoni Charles mwananchi aliyesaidia kutoa mwili wa marehemu ndani ya maji ya bwawa hilo wameiomba serikali kuwasisitiza wenye mabwawa na serikali kuweka uzio katika maeneo yote yenye vyanzo vya maji kwa usalama wa raia na mali zao.

Sauti ya shuhuda wa tukio
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kabanga wakiwa katika msiba wa Rashid Paul

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kabanga Kata ya Lulembela amekiri kuwepo kwa tukio hilo nakuwataka wamiliki wa mabwawa ya kunyweshea mifugo na shughuli za umwagiliaji kuzingatia uwekaji wa uzio katika maeneo yao, huku akibainisha mikakati ya kijiji katika kufuatilia suala hilo ili lizingatiwe kwa wakati.

Sauti ya mwenyekiti wa kijiji Kabanga