TAMISEMI yatoa maagizo kwa mkandarasi Geita
1 September 2024, 9:11 pm
Kusuasua kwa mkandarasi anaetekeleza ujenzi wa mradi wa TACTIC wa barabara zenye urefu wa kilometa 17 TAMISEMI yatoa tamko.
Na Evance Mlyakado – Geita.
Licha ya serikali kutenga bajeti ya zaidi ya bilioni 22 kwaajili ya ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 17 kwa kiwango cha lami katika kata nne zilizopo mjini Geita bado ujenzi wa mradi huo unasuasua kutokana na mkandarasi anayetekeleza mradi huo kushindwa kuendana na kasi inayotakiwa kwa mujibu wa mkataba.
Mradi huo unaotekelezwa kupitia ufadhili wa benki ya dunia unapaswa kukamilika ndani ya miaezi 15 ambapo mpaka sasa miezi tisa imepita lakini bado mradi huo umetekelezwa kwa asilimia 34 jambo ambalo limepelekea naibu katibu mkuu wa ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila kufika katika mradi huo na kumuagiza mkandarasi kukamilisha mradi huo kabla ya mwezi februari 2025.
Sauti ya naibu katibu mkuu TAMISEMI Mhandisi Rogatus Mativila
Kwa upande wake Mkurugenzi anayesimamia mradi huo katika mji wa Geita Mhandisi Lukasi Nyake amesema mkandarasi huyo ameshapatiwa ushauri wa kitaalamu zaidi ya mara 45 lakini bado hali ya mwenendo wa mradi huo inaendelea kuwa mbaya.
Sauti ya mkurugenzi anayesimamia mradi Mhandisi Lukas Nyake
Nao wananchi wamebainisha changamoto wanazozipata kutokana na mradi huo kutokamilika kwa wakati.
Sauti za wananchi