Storm FM

Akiba atelekeza mke na watoto watatu

1 September 2024, 8:45 pm

Moja ya eneo la mji wa Geita kwa juu. Picha na Evance Mlyakado.

Licha ya serikali kuendelea kupambana kukomesha vitendo vya ukatili katika jamii lakini vitendo hivi vinaonekana kuendelea kujitokeza katika maeneo mengi hasa ya vijijini Mkoani Geita

Na Evance Mlyakado -Geita.

Mwanaume mmoja mkazi wa Nyantorotoro A anadaiwa kutekeleza Familia ya Mama na watoto watatu Kwa miaka Tisa bila huduma yoyote huku akidaiwa kufanya vurugu na Vitisho Kwa Mama huyo na watoto wake.

Akizungumza na storm fm Agosti 23,2024 Veronica Julius akiwa na watoto wake watatu walisafiri kutoka Nyarugusu hadi myantorotoro A kata ya Nyankumbu anapoishi Akiba na mke wake mpya, Mapokeo ya mwanaume yakawa mabaya hali iliyopelekea kuibuka kwa ugomvi mbele ya balozi wa eneo hilo.

Sauti ya Veronica Julius ambaye ni mama wa watoto hao watatu.

Veronica Julius anasema kilichomsukuma kuja nyumbani hapo ni Msukumo na kiu ya Watoto wake kutaka kumuona Baba yao mzazi.

Sauti ya Veronica Julius

Kwa Upande wake Mke wa Sasa wa Bwana Akiba Mary Benjamin anasema aliamua kuipokea familia hiyo kama Mwanamke na mama wa watoto licha ya kwamba Mme wake hakutaka wasipokelewe nyumban hapo.

Storm Fm ilifanya jitihada za kumtafuta Bwana Akiba ili kufahamu ukweli wa madai ya Veronica Julias ambaye alikiri kumfahamu Veronica Julius huku akisema kuwa Mwanamke huyo amekuja kuharibu familia yake tu kwasasa.

Sauti ya Akiba

Balozi Valence ni Kiongozi wa eneo hilo ambapo anaishi Akiba na Familia yake mpya amethibitisha kutokea kwa ugomvi nyumbani kwa Akiba.

Sauti ya balozi wa eneo hilo

Kwa upande wake Lameck Hazina ambaye ni Afisa Mtendaji wa mtaa wa Nyantorotoro A amezungumza na mlalamikiwa na kutokana na hali ya mwanaume kupuzia wito wake hivyo akaandika barua kwenda Dawati la jinsia ili kupata msaada zaidi.

Sauti ya Afisa mtendaji na Mwenyekiti wa mtaa wa Nyantorotoro A

Tukio hili limetokea Ijumaa ya Agosti 23,2024 majira ya saa 12 jioni nyumbani kwa Akiba.