Storm FM

CCM wilaya ya Geita yatoa tamko ufatiliaji wa miradi

22 August 2024, 4:45 pm

Pikipiki ambazo zimekuwa zikitolewa na CCM kwaajili ya kufanya ufatiliaji wa miradi ya chama. Picha na wikipedia

CCM wilaya ya Geita kuwachukulia hatua baadhi ya wajumbe ambao wamekuwa wakitumia pikipiki  za chama hicho kusafirisha abiria jambo ambalo ni kinyume na malengo.

Na: Kale Chongela – Geita

Katibu wa CCM wilaya ya Geita ndugu Marko Msuya leo Agosti 22, 2024 akiwa ofisini kwake amesema wamebaini kuna baadhi ya wajumbe wamekuwa wakihujumu kwani lengo la kutoa pikipiki hizo ni kwajili ya kufuatilia miradi ambayo imetekelezwa na chama hicho na si vinginevyo.

Sauti ya katibu CCM

Mwenyekiti wa egesho la madereva pikipiki mtaa wa Shilabela kata ya Buhalahala mjini Geita Bw. Reuben Edward amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo kwa baadhi ya maeneo

Sauti ya mwenyekiti

Baadhi ya madereva pikipiki  katika halmashauri ya mji wa Geita wamebainisha kuwa hali hiyo ya baadhi ya wajumbe kutumia pikipiki za chama kinyume na matarajio imekuwa ikiibua sintofahamu na kwamba ni bora pikipiki hizo zifanya kazi ambayo imepangwa ya kukagua miradi.

Sauti ya madereva