Storm FM

Inatisha, avunjika uti wa mgongo, aomba msaada

22 August 2024, 3:56 pm

Baadhi ya vidonda ambavyo vipo sehemu za makalio yake kutokana na kukaa kwa muda mrefu. Picha na Evance Mlyakado

Annastazia Jacob (22) mkazi wa kijiji cha Mabamba, kata ya Nyamigota ndani ya mamlaka ya mji mdogo wa Katoro wilayani na mkoani Geita anapitia maumivu makali na mateso baada ya kuanguka kutoka juu ya mti.

Na: Evance Mlyakado – Geita

Changamoto hiyo imesababisha ashindwe kutembea, kusimama wala kukaa kwa muda wa miaka miwili sasa na kushindwa kufanya shughuli za uchumi jambo ambalo limepeleka vidonda kwenye makalio yake baada ya kukaa kwa muda mrefu na kutoa haja kubwa na ndogo bila kujitambua.

Annastazia Jacob anahitaji msaada wa hali na mali kutoka kwako ili aweze kupata matibabu na kurejea katika hali yake ya kawaida kwani baada ya tatizo hilo alitelekezwa na mume wake Changia kupitia namba 0756397026.

Sauti ya Annastazia
Mazingira ya chumba cha Annastazia ambacho hutumia kukaa na kulala. Picha na Evance Mlyakado

Baba mlezi na dada wa Anastazia wamesema tangu kuumia kwake wamejitahidi kumpeleka katika matibabu mbalimbali ikiwemo dawa za asili kutokana na hali ngumu ya kiuchumi.

Sauti ya ndugu

Baadhi ya viongozi wa eneo analoishi Annastazia wameiomba jamii na watanzania kuendelea kujitokeza kumsaidia katika matibabu yake.

Sauti ya viongozi wa kijiji cha Inyala

TUMA MSAADA WAKO KUPITIA – 0756397026