Storm FM

Mikopo yenye riba nafuu kuwainua wananchi Geita

17 August 2024, 1:19 pm

Mgeni rasmi akiwa na baadhi ya watumishi katika zoezi la kukata utepe kuashiria uzinduzi. Picha na Kale Chongela

Kufuatia kukua na kuimarika kwa maendeleo ya teknolojia nchini kumewezesha wananchi wengi kupata huduma za kibenki kwa njia salama na kuwa na uhakika wa usalama wa fedha zao.

Na: Kale Chongela – Geita

Afisa mtendaji mkuu wa Benki ya mwalimu (MCB) Richard Makugwa jana Agosti 16, 2024 ameshiriki katika uzinduzi wa tawi la benki hiyo mkoani Geita ambapo amesema kuwa uzinduzi huo umelenga kusogeza huduma kwa wananchi.

Sauti ya afisa mtendaji mkuu
Baadhi ya walimu na wanachama wa CWT mkoa wa Geita wakiwa katika shughuli ya uzinduzi wa tawi la MCB. Picha na Kale Chongela

Kaimu Katibu  mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) Joseph Msalaba amebainisha kuwa huduma za kibenki zitawawezesha walimu kupata fursa mbalimbli ikiwemo kupata mikopo yenye riba nafuu.

Sauti ya katibu CWT

Mwakilish

Mwakilishi wa katibu tawala Elfas Msenya akizungumza kwa niaba ya katibu tawala mkoa wa Geita  mara baada ya kuzindua tawi hilo ameahidi kuendelea kutoa kipaumbele kwa wawekezaji ndani ya mkoa wa Geita.

Sauti ya mwakilishi katibu tawala